Luke 2:4-7

4 aHivyo Yusufu akapanda kutoka mji wa Nasiri ulioko Galilaya kwenda Uyahudi, mpaka Bethlehemu, mji wa Daudi, kwa sababu yeye alikuwa wa ukoo na wa nyumba ya Daudi. 5 bAlikwenda huko kujiandikisha pamoja na Mariamu, ambaye alikuwa amemposa naye alikuwa mjamzito. 6Wakiwa Bethlehemu, wakati wa Mariamu wa kujifungua ukawa umetimia, 7 cnaye akamzaa mwanawe, kifungua mimba. Akamfunika nguo za kitoto na kumlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hapakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni.

Wachungaji Na Malaika

Copyright information for SwhKC